Bongo Movie

Kanumba Day: Wasanii wa filamu wamlilia Steven Kanumba

Ukiwa huu ni mwaka wa 4 toka tasnia ya filamu impoteze staa wa filamu, Steven Kanumba, Alhamisi hii (April 7) wanafamilia, ndugu, jamaa pamoja na marafiki, walifanya ibada kwa pamoja katika kaburi la Kanumba Kinondoni.
Jacline

Ibada hiyo ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa filamu, Mama Kanumba, Mama Elizabeth Micheal pamoja na mashabiki mbalimbali wa filamu.

Pia wasanii mbalimbali wa filamu kupitia mitandao yao ya kijamii, walitoa ya moyoni juu ya kumpoteza nguli huyo wa filamu.

Shamsaford
Hello, our hero, we miss u so much nobody can replace u inside our heart we love u
????????may God rest u’re soul in peace

Auntyezekiel

Ntakuwa ni muongo na mnafiki kama siwezi kushukuru na kutambua mchango wa huyu mtu katika maisha yangu, maana nilianza kama utani kupitia yeye haswa kazi hii ya ‘YOUNG BILLIONER’ niliweza tambulika sio tu ndani bali hata nje ya Tanzania. Ni kama mshumaa uliyopulizwa na upepo tena wa bahari. Umeondoka ikiwa tasnia nzima tunakuangalia wewe kama nguzo yetu na msaada wetu mkubwa kutoka hapa tulipo kwenda hatua nyingine mbele na kamwe pengo lako halitazibika hata atokee nani katika tasnia hii hata nipewe siku nzima ya leo (jana) siwezi maliza sifa zako. Popote pale ulipo jua kwamba umetuachia pengo kubwa sana sanaaa kwa miaka hii 4 tuu usiyokuwa nasi tumejua na kukiri uthamani wako ni mkubwa katika filamu za Tanzania. Tulikupenda Mungu amekupenda zaidi upumzike kwa amani Kanumba wetu…….I love u so much.

Steve Nyerere

Tukatae tubishe king kaondoka na sanaa yake. Sasa hivi zipo chuki, kuchekeana kichina . So sijaona mwana harakati kama Kanumba anayeweza kuthubutu kwenye mambo mbali mbali ya sanaa. Wengi wameridhika na hela ya mboga gari basi. Sio kutanua soko kuwa la kimataifa. Kanumba aliitangaza tasnia ndani na nje . Kanumba kanumba kanumba kanumba duh! sitaki sema meengii pumzika mzaziiiiiiii da ngumu kuwa mbali nawe lakini kila jambo anapanga mungu. uku mambo yale yale amna mabadiliko ukiwa na wenzako mmekaa usiache chakula kwenda msalani ama soda ohooooooooooo itakula kwako

Wastara

Miaka 4 sasa bado jina lako alijafutika midomoni mwetu na halitafutika kamwe. Tunaokuombea.

JB
Bado tuna kukumbuka…pumzika kwa amani ‪#‎4years‬# marehemu steven kanumba#

Ray Kigosi

The Great pumzika kwa amani Mwenyezi Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi. Kila nafsi itaonja umauti. (rip the great pioneer songa mbelE ncha ya kisu haipigwi konzi) huu ulikuwa msemo wake mkubwa pumzika kwa amani broo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents