Burudani

Roma: Kupotea kimuziki kunasababishwa na vitu vingi, sio ndoa

Rapper ambaye anafanya vizuri kwenye Hip Hop ya Bongo, Ibrahim ‘Roma’ Mussa, amefunguka na kusema kuwa si kweli kwamba msanii akioa au kuolewa anapotea kwenye tasnia muziki.

harusi-roma-559x520

Akiongea na Bongo5, Roma aliyefunga ndoa wikiendi iliyoisha, amedai kuwa huo ni mtazamo tu wa watu lakini hamna ukweli wowote.

“Kila mtu ana mtazamo wake katika hilo suala huenda wapo sahihi na hoja zao na kupotea kwenye muziki kunasababishawa na vitu vingi sana. Kuna watu wamepotea katika muziki wapo mabachelor tu wamekuja katika game na wamepotea,” amesema. “Kwahiyo sidhani kama hao nao walikuwa wameoa, ni uoga wao tu kutokana hizo hoja zao. Kuna muda wasanii wanapotea kwenye game kwa kukosa ubunifu na sapoti na mifano ipo, wasanii wakali wanaimba vizuri hawapewi sapoti mtaani tunaona wanapotea,” ameongeza.

“Kwangu hamna kigeni labda zaidi ya sherehe na watu walikuja pale wakala pilau na vinywaji basi maana mtu ambaye nimemuoa nipo naye tokea na wimbo mmoja tu hadi tukafanikiwa kupata mtoto anaitwa Ivan ambaye sasi hivi ana miaka minne. Kwahiyo ni Roma yule yule tu, zaidi mengi niliyoongea sasa hivi yanafanyiwa kazi wafanyakazi hewa,mara tunaona tumbili wanasafirishwa ndio hayo sasa hivi Mh. Rais anatumbua majipu. Na mimi kama Roma nampongeza sana Mh. Rais kwa kutumbua majipu zaidi, apewe tu ushirikiano.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents