Burudani

Safari ya matumaini ya wasanii wa Bongo

Kiukweli wasanii wa Bongo ni watoto yatima wanaohitaji pongezi kwa kujituma kwao. Serikali kelele nyingi lakini hakuna ninachokiona zaidi ya kuwapongeza wakileta tuzo na kuwakaribisha bungeni, then wakitoka msoto wao unabaki pale pale.

Wasanii wote walipanda jukwaani kuonesha upendo wakati Juma Nature alipo kuwa akifunga Show

Kama kweli serikali inadhani inawasaidia wasanii hebu angalia hii safari yao then uniambie kama kweli wamesaidiwa kitu. Kwanza walianza kuzuiwa wasifanye muziki sababu ni uhuni lakini wakakaza hadi wazee wakaelewa, hii ilikuwa vita ya kifamilia.

Baadaye wakaanza kuuza album zao kwenye kanda na CD bahati mbaya mfumo kuwa rahisi zaidi kwa wezi/majangili wa kazi za sanaa kuliko msanii kuingia MJ Records na Bongo Records kurekodi. Naskia ingechukua miezi 6 kupata chance kwa Master J au P- Funk ila ingechukua sekunde tu mtu kuandika bango lake “TUNABURN CD HAPA”na serikali yao ikachukulia poa.

Yalipowafika shingoni mwisho wakaamua kutotoa album kabisaa.

Haya likaja jingine ‘Tushoot video kali ili tushindane kimataifa.’ Kuomba kibali airport ili ushoot scene ya dakika mbili utafuatilia mwezi na nusu. Wakaona isiwe tabu Mzee Madiba alishaona fursa akaweka njia rahisi kwa vijana wake wanaofanya sanaa so inabidi wakadandie pipa kushoot location za south na umekuwa mtindo sasa.

Hatujakaa vizuri video queen wa kibongo nao miyeyusho,ukimtaka mkashoot video,miyeyusho kibao,kwanza hawana kampuni zinazoeleweka za models (nyingi zipo instagram) kwahiyo inabidi udeal na mtu mmoja mmoja mara ooh..sina passport, mara hapatikani, wazazi hawataniruhusu nivae nguo fupi, yaani full stress.

Mwisho naona wasanii wetu mmeamua isiwe tabu,sasa hivi ni mwendo mdundo mademu wa kizungu na machotara kwenye videos. Diamond, Ben Pol, Shetta, Rich Mavoko, AY, Alikiba Joh Makini na wengi walioshoot SA wametumia mademu wa kule.

Baada ya msoto huo wote hapo ndipo tunapoona mkono wa serikali ukisema “FUNGIA HII VIDEO HAINA MAADILI.”
Tumia akili ya kawaida tu.

Mpishi katoka China,malighafi ya chakula, China,jiko linapopikiwa lipo China,nyama ya China, unategemea kuletewa makande? Subiri ule vyura na mijusi tu, wala usilaumu relax kabisa. Director, location,video queen na kila kitu vya SA halafu unategemea video yenye maadili ya kibongo?

Simlaumu msanii yeyote kwasababu muziki ni biashara na bado mzubao ni mkubwa kuanzia kwa serikali hadi mtu mmoja mmoja. Nahisi tumelala, Bongo Flava, imekua ghafla na fursa zimekuwa nyingi tumeshindwa kuzitumia tunawapa wajanja wa South na Marekani.

Nashangaa juzi wamekuja na issue za Mirabaha,sipingi hilo lakini ninachokiona mimi pale kuna watu waliona kuna ulaji wa moja kwa moja na serikali ilisapoti kwasababu ilikuwa inapata mapato. Ninachoshauri serikali isikimbilie kutafuta kuingiza hela kupitia wasanii hawa ghafla tu. Ijitolee kwanza kurahisisha baadhi ya mambo sababu hapa Bongo Flava ilipo kuna watu(wasanii wenyewe) walijitolea kufanya kazi bure ili kupush hizi harakati.

Sasa unapokuja unakuta mtu kalemewa na mzigo mzito wa misumari,moto,mawe,kokoto na ndizi halafu unaanza kumtua mzigo wa ndizi sababu unataka upate chakula,siyo sawa hata kidogo.

Poleni na hongereni wasanii wa Bongo, msife moyo, wataelewa tu.

Imeandikwa na Grayson Gideon producer wa Planet Bongo East Africa Radio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents