Burudani

Baby Madaha awashangaa wasanii wa kike wa filamu wanaohangaika na Serengeti boys

Msanii wa filamu Bongo, Baby Madaha amesema kuwa na mpenzi mwenye umri mdogo kwake haoni kama kuna faida yoyote.

Baby-Madaha

Wasanii wa kike wa filamu Bongo wameonekana kuanzisha style mpya kwa kuwateka kwenye mahusiano wasanii wadogo wa muziki na kuwaingiza kwenye himaya zao za mapenzi kama ilivyokuwa kwa Shilole na Nuh Mziwanda, Nisha na Baraka da Prince, Jacquline Wolper na Harmonize, na sasa ikidaiwa kuwa Raymond tayari kashanasa kwenye mtego wa Nisha.

Akiongea na gazeti la Mtanzania, Baby Madaha alisema, “Sijawahi kuwaza kama nitakuwa na Serengeti boy kwangu hawana nafasi sioni faida yoyote kwao, mimi nawashangaa kwa kuwa wengi wao wanatafuta umaarufu hakuna mapenzi wala maisha endelevu hapo.”

Aidha Baby amewataka wasanii wenzake kuwa na wanaume wenye umri wao ama wawe na wanaume watu wazima kama wanataka kulinda heshima zao na kujiongezea mashabiki badala ya kuwa na wanaume wenye umri mdogo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents