Michezo

Samatta azungumzia ‘game’ yao Vs Liverpool ”Tanzania kila mmoja ataufuatilia, wanasema lazima nifanye kitu dhidi ya Van Dijk”

Hapo kesho majira ya saa nne za usiku Mtanzania Mbwana Samatta atashuka dimbani akiwa na kibarua kizito cha kukabiliana na miamba ya soka kutoka England timu ya Liverpool kwenye michuano ya UEFA Champions League.

Genk striker Ally Mbwana Samatta is a boyhood Manchester United fan born in Tanzania

Samatta ambaye ni Mtanzania pekee aliyepata bahati ya kucheza michuano hiyo mikubwa kabisa barani Ulaya, anatarajiwa kushuka uwanjani huku akiwa na jezi yake ya rangi ya Blue ikiashiria kuwa wapo nyumbani na klabu yake ya KRC Genk huku akiwapatia furaha watazamaji watakao kuwa wanaufuatilia mchezo huo.

 

Katika kuelekea mchezo huo mshambuliaji huyo amezungumza na vyombo vya habari na kuweka wazi malengo yao kama timu huku akisema kuwa Watazania hivi sasa wanauzungumzia mechi hiyo ya kesho, wakimzungumzia yeye dhidi ya beki bora kwa sasa duniani (Virgil) Van Dijk, huku wakimtaka afanye kitu.

Samatta (left) says facing United's rivals Liverpool in the Champions League is a 'dream game'

”Wakati nilipokuwa mdogo nilikuwa nikiishabikia Manchester United, lakini kwa sasa hatuzungumzii Manchester United bali ni Liverpool,” amesema Samatta.

”Tunaamini Liverpool ni timu imara kwa sasa katika Premier League na hata kwenye michuano ya European, hivyo tunatarajia mchezo utakuwa mgumu. Tunacheza mbele ya mashabiki wetu hivyo tunahitaji tuwe wenye furaha mwishoni mwa mchezo. Hivyo tutafanya kwa uwezo wetu wote.”

 

”Nchini Tanzania, kila mmoja atakuwa anaufatilia huo mchezo wa kesho, wananizungumzia mimi na Van Dijk. Wanasema nilazima nifanye kitu dhidi yake, niende mbele yake, ni ‘dribble’, nafikiria mambo mengi sana juu yao.”

 

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents