Michezo

Samatta kupimana ubavu na Mo Salah, nani ataibeba timu yake usiku wa leo UEFA Champions League

Wachezaji nyota kutoka barani Afrika ambao wanakipiga Ulaya, Mo Salah, Mane na Mbwana Samatta hii leo watakutana katika mchezo wa UEFA Champions League  ambapo kila mmoja akijaribu kuitetea klabu yake.

Samatta tayari ameshafunga goli moja kwenye michuano ya Champions League

Samatta ambaye ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania atakuwa nyumbani na klabu yake ya KRC Genk kuikabili Liverpool mchezo wa kundi E.

Liverpool ni mabingwa watetezi kwenye michuano hii, baada ya kuwachapa Tottenham hatua ya fainali msimu uliopita.

Hata hivyo mabingwa hao wanashika nafasi ya pili kwenye kundi lao, baada ya kuwa na pointi 3 wakati Genk ikiburuza mkia kwa kuwa na alama 1.

Image result for Samatta vs Mo Salah

Mohamed Salah amerejea kwenye kikosi cha Livepool baada ya kupona majeraha yake ya kifundo cha mguu. Mshambuliaji huyo wa Misri, 27 alipata jeraha hivyo kukosa mechi ya Liverpool na Manchester United siku ya Jumapili.

Katika michuano iliyopita ya Ulaya, Genk ilikutana na Chelsea Stamford Bridge mwaka 2011-12 katika hatua ya makundi, na kutoka sare ya 1-1 nyumbani na baadaye kupoteza bada ya kuchapwa na Chelsea mabao 5-0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents