Michezo

Sancho avalia njuga kutua United

Jadon Sancho anamshinikiza wakala wake kuhakikisha anafanikisha dili lake la uhamisho wa kutua Manchester United baada ya kushindikana msimu uliyopita.

Jadon Sancho wants to return to the Premier League with Man Utd |  GiveMeSport

Winga huyo wa Borussia Dortmund ameonekana kutoridhishwa na namna anavyowakilishwa na wakala wake Mnigeria, Emeka Obasi katika kufanikisha usajali wake wa kwenda United.

Sancho mwenye umri wa miaka 21, alishindwa kujiunga na United msimu uliyopita na hivyo ameamua kulivalia njuga swala hilo la usajili kwa kumuhimiza wakala wake kukamilisha dili hilo msimu huu.

United wanaonekana kama kukata tamaa kumsajili nyota huyo msimu huu wa majira ya joto kutokana na bajeti yao lakini pia kwa kufanikiwa kwao kumuongezea kandarasi mshambuliaji wao  Edinson Cavani.

Dortmund wamethibitisha kuwa wanachotaka wao ni fedha taslimu na sio nusu nusu kwa usajili wa Sancho, hukukandarasi yao ikitarajiwa mwaka 2023.

Thamani ya Sancho ilikuwa ni paundi milioni 108 mwaka jana lakini Dortmund wanaonekana kama kulegeza kamba mwaka huu hasa kutokana na kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Corona. Mpaka sasa winga huyo wa Uingereza ameshafunga jumla ya magoli 14, assists 18 kwenye michezo 35.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents