Siasa

Mke wa Mugabe ashtakiwa kwa kufanya mazishi ya rais Mugabe kinyume na tamaduni

Mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe,ameagizwa kufika mbele ya mahakama ya kitamaduni kwa tuhuma za kufanya mazishi “yasiyofaa” ya hayati Rais Robert Mugabe.

Grace Mugabe anatuhumiwa kwa kuenda kinyume na utamaduni wa jamii yao kwa kumzika mume wake katika boma la familia badala ya kumzika “sehemu iliyochaguliwa na jamaa zake na mama yake”.

Katika waraka kutoka kwa Chifu Zvimba, ambaye ni mkuu wa kitamaduni wa nyumbani kwa kina Mugabe, Mke wake Grace anatakiwa kuufukua mwili wa hayati Rais Mugabe ili uzikwe tena “kulingana na utamaduni wa watu wa Zvimba”.

Pia ameagizwa kulipa faini ya ng’ombe na mbuzi kwa kukiuka utamaduni.

Mugabe alifariki mwaka 2019 katika hospitali moja nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95.

Familia yake iliamua afanyiwe mazishi ya faragha kijijini kwao Kutama wilaya ya Zvimba- karibu kilomita 90 sawa na (maili 55) magharibi mwa mji mkuu wa Harare – baada ya mvutano wa wiki kadhaa na serikali.

Patrick Zhuwao, mpwa wa marehemu rais, siku ya Alhamisi aliiambia televisheni ya Shirika la utangazaji la Afrika Kusini kwamba Mugabe alizikwa kulingana na ombi lake, uamuzi ambao unastahili kuheshimiwa.

Amesema hakuna mzozo ndani ya familia akiongeza kwamba suala hilo lipo nje ya mamlaka ya chifu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents