Michezo

Serge Aurier asaidia kuokoa maisha ya mchezaji wa Mali

Mchezaji wa klabu ya Paris Saint-Germain kutoka Ivory Coast Serge Aurier ambaye anacheza nafasi ya beki amesifiwa sana baada ya “kuokoa maisha” ya mchezaji wa Mali Moussa Doumbia Jumamosi.

3953fc3b00000578-3834327-image-m-33_1476273369560
Aurier (kati) akimsaidia Moussa Doumbia baada ya kuanguka ghafla

Doumbia ambaye alianguka ghafla na kupoteza fahamu.

Aurier aliingia kati baada ya kuona mchezaji huyo wa Rostov alikuwa anakaribia kumeza ulimi akamlaza kwa upande na kumzuia kuumeza ulimi wake.

Kocha wa Mali Alain Giresse amesema alizungumza na Aurier baada ya mchezo huo na kumshukuru.

“Wachezaji wote waligundua kwamba Doumbia alikuwa anakabwa kooni na kushindwa kupumua na alikuwa karibu kuumeza ulimi wake,” Giresse, aliiyambia redio ya Ufaransa ya RMC.

“Ni hapo ambapo Aurier, akiwa na mmoja wa wachezaji wetu, alichukua hatua haraka wakamlaza upande na kuutoa ulimi wake, kwa sababu alikuwa anakaribia kupoteza maisha.”

Katika mechi hiyo Ivory Coast walishinda 3-1 mchezo wakuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents