Habari

Serikali kula sahani moja na polisi wanaonyanyasa watuhumiwa

Serikali imesema hatua kali zitachukuliwa kwa askari polisi wanaowanyanyasa watuhumiwa wa makosa mbalimbali kinyume na sheria.

x4-3-jpg-pagespeed-ic-02tg8_bjsn

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Hamad Masauni, Jumatano hii bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililohoji hatua zinazochukuliwa kwa matukio kama hayo.

“Serikali inatambua inawezekana kuwepo kwa malalamiko katika vituo vyetu vya polisi kwa mujibu wa PGO namba 103(1) lazima kamanda achunguze na kuangalia ukweli wa malalamiko hayo kama yana ukweli ndani yake akibainika askari aliyefanya kitendo hicho atachukuliwa hatua za kinidhamu dhidi yake kama vile kukatwa mshahara au kufukuzwa kazi,”amesema Masauni.

“Serikali kupitia jeshi la polisi limeweka mfumo madhubuti wa kushughulikia malalamiko hayo ya mikoa yote ya polisi makao makuu ya polisi kama haitoshi wizarani kwangu kuna madawati la kushughulikia malalamiko. Kwa nafasi hii nitoe raia ambao hawatendewi haki wafuate utaratibu huo na hatua zitachukuliwa kikamilifu,”ameongeza.

“Pia jeshi la polisi limeendelea kutoa elimu kupitia mfumo wa mafunzo kazini,vilevile mafunzo ya vitendo ili kuhakikisha askari wao wanafanya kazi kwa weledi na usasa kwa kuzingatia sheria na nchi.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents