Habari

Serikali kuongeza viwango vya pango la ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi, William Lukuvi amesema kuwa serikali itaendelea kuongeza hazina ya ardhi kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo, wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendelea ya Makazi kwa mwaka wa Fedha kwa mwaka 2017/2018 , Bungeni mjini Dodoma na kutangaza ongezeko la pango la Ardhi kwa mashamba nchini.

“Serikali inakusudia kuongeza viwango vya pango la ardhi kutoka shilingi mia 400 hadi shilingi 1000 kwa hekari kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7 kwa mashamba ya biashara kwa mwaka yaliopimwa na kumilikishwa nje ya miji kiwango kinachotozwa leo cha shilingi miliono 400 kwa hekari 1 ni ndogo sawa na ikilinganishwa na thamani ya pamoja na uwezo wa uzalishaji husika,” alisema Lukuvi.

“Hapa sina maana ya wakulima wadogo wadogo maskini wenye hati za kimila wale wenye hati za kimila watatozwa sifuri sifuri hawatozwi kodi yoyote.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents