Habari

Serikali yaagiza sukari tani laki moja kutoka nje

Serikali ya Tanzania imeagiza sukari tani 131,000 ili kukabiliana na upungufu uliopo kwa sasa nchini, na pia kuelekea katika mfungo wa Ramadhani.

katika kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu bungeni leo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekikiri kuwepo kwa upungufu wa sukari nchini kitu kinachopelekea bei kupanda baadhi ya maeneo na kusema tayari serikali imechukua hatua mbalimbali ili kumaliza tatizo hilo.

Majaliwa amesema matumizi ya sukari nchini kwa mwaka yanafika tani laki 420 na uzalishaji wa ndani ni tani 131, hivyo haufiki kiasi hicho hivyo kusababisha upungufu wa sukari nchini lakini tayari wameagiza tani 131,000 nje ya nchi.

“Tumeshachukua hatua kwa kuagiza tani laki 131 za sukari, tani elfu 80 tayari zimeshaingia nchini na tani elfu 35 zimeshaanza kusambazwa maeneo mbalimbali nchini,” amesema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa sukari hasa katika kipindi hiki ambacho waumini wa dini ya Kiislamu wananataraji kuanza mfungo wa Ramadhani.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents