Habari

Serikali yakusudia kuunda kamati ya kuisaidia Taifa Stars

Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania kuitandika Morocco 3-1 na kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye michuano ya kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia 2014, jana serikali kupitia naibu waziri Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla imesema itaunda kamati ili kuisaidia Taifa Stars kushinda katika michezo mitatu ijayo ili kujiwekea nafasi nzuri ya kushiriki kombe la dunia mwaka 2014.

Makalla

Akizungumza na vyombo vya habari jana, Makalla aliipongeza Taifa Stars kwa ushindi ilioupata kwakuwa imeijengea heshima Tanzania na kuwataka wachezaji waongeze bidii.

“Serikali inakusudia kuunda kamati ya kusaidia Taifa Stars ili kuongeza nguvu haraka iwezekanavyo ili kuiwezesha kufanya vema katika mechi zilizobaki. Pamoja na kamati serikali itaendelea kulipa mshahara wa kocha wa timu ya taifa, alisema Makalla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents