Habari

Serikali yapigilia msumari sheria ya ndoa za utotoni (+video)

Naibu waziri ya Afya, Jinsia,Wazee, na Watoto Mhe. Hamisi Kigwangalla amesema hairuhusiwi mtoto yoyote kuoa au kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari.

Hayo yamezungumzwa na Mhe. Kigwangalla leo, Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la muheshimiwa Faida Mohamed Bakari Mbunge wa Viiti Maalum liliohoji.

Sheria nyingi nchini hususan zile zinazohusu haki za wanawake zimepitwa na wakati na hivyo kuwanyima haki wanazostahili wanawake, Je ni sheria zipi zinazowanyima haki wanawake na watoto nchini?

“Sheria ya mwaka 1971 katika kifungu cha 13 na kifungu cha 17 zinaruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo wa miaka 14 au 15 kwa ridhaa ya wazazi au kwa amri ya Mahakama, vifungu hivi humyima mtoto haki zake za msingi . Mapendekezo ya sheria ya ndoa na miradhi tayari yameshawasilishwa kwenye wizara ya sheria na katiba pamoja na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi na taratibu zote zikiisha mswada utawasilishwa bungeni,” alisema Dr Kigwangalla.

“Aidha katika jitihada za kukomesha ndoa za utotoni mwaka 2016 serikali iliifanyia marekebisho sheria ya elimu ya mwaka 1978 ili kuzuia watoto wa shule wasiolewe kwa mujibu wa sheria hii namba 4 ya mwaka 2016 kifungu cha 60 kifungu kidogo cha kapito (a) hairuhusiwi mtoto yoyote kuoa au kumpa mimba ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kwa kuwa sheria hii inalenga ulinzi kwa watoto walio mashuleni.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents