Habari

Updates: Tabasamu zatawala majeruhi wa Lucky Vicent wanaotibiwa Marekani

Majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent waliopelekwa kutibiwa nchini Marekani, inaripotiwa hali zao kuendelea vizuri huku Sadia na Wilson wamepelekwa kwenye kituo maalumu kwa uangalizi wa karibu na Doreen ameendelea kuwepo katika wodi ya watoto Mercy Hospitalini.

Doreen

Taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, imeeleza mtoto Sadia kuendelea vizuri sana pamoja na maeneo mengine ya mwili aliyoumia na kuvunjika, Sadia alikuwa amevunjika shingo, na kupitia maumivu makubwa ya wiki sita kabla ya shingo yake kurejea hali yake ya kawaida.

Kama ilivyoripotiwa hapo nyuma, Sadia na Wilson wamepelekwa kwenye kituo maalumu kwa uangalizi wa karibu, mjini Sioux City, katika Jimbo la Iowa, na wanaendelea vizuriI.

Sadia

Doreen ameendelea kuwepo katika wodi ya watoto Mercy Hospitalini, ameelezewa kuendelea kuimarika na mwili wake kuitikia matibabu anayoendelea nayo. Doreen alifanyiwa upasuaji kwenye nyonga (Chini ya Kiuno), kwenye bega, kwenye kidevu, na mwisho kwenye uti wa mgonga.

 

 

Wilson ameanza kusimama na kutembea mwenyewe kwa msaada wa fimbo ya kutembea.

 (Picha kwa Hisani ya DMS, Sioux City) 

 

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents