Habari

Serikali yazungumzia tukio la mwanafunzi wa kike wa Tanzania kuvuliwa nguo India

Serikali ya Tanzania imesema kuwa inaendelea kufatilia ili kuchukua hatua zaidi juu ya matukio yalitokea nchini India katika chuo cha Acharya Bangalore, ikiwemo la mwanafunzi wa Kike kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo.
maige20
Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige

Akitoa tamko la Serikali leo Bunge Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige amesema tayari serikali imeshapeleka dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya india ili kuonyesha kukasirishwa na kitendo hicho.

Balozi Maige ameongeza kuwa tayari wameitaka serikali ya India kuchukua hatua za kipolisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kupeleka ulinzi wa kutosha katika maeneo wanaoishi wanafunzi hususani wa kitanzania ambapo leo kumeri kwa mtu anaesadikiwa kuwa mtanzania kufariki katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa upande wa baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuwa na tamko rasmi la kuonyesha kuchukizwa na ubaguzi kwa watanzania pindi waendapo kuishi nje ya Tanzania.

Tukio hilo limekuja baada ya Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore kuripoti kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa india mkazi wa Hessaraghata aliekuwa na Mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.

Wakati huo huo Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.

Source:EATV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents