Habari

Shika Ndinga 2018 yatimua vumbi Mwembe Yanga Dar

Wakazi wawili wa Dar es salaam, wameibuka washindi katika shindano la shika ndinga lililoendeshwa na kituo cha Radio cha Efm.

Meneja Mkuu E-fm DennisSsebo akikabidhi kadi ya pikipiki kwa Ndg. Abas Awadhi mshindi wa bodaboda kupitia ShikaNdinga2018 kwa upande wa wanaume.

Washindi hao ni Ashura Ramadhani mkazi wa Bunju ambaye alipiga simu na kupata nafasi hiyo kupitia kipindi cha uhondo.

Mwingine ni Abbas Awadhi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala ambaye alipata nafasi ya kushiriki katika shindano hilo kupitia kipindi cha Genge kinachoendeshwa na radio Efm.
<img src="http://bongo5.com/wp-content/uploads/2018/04/Screen-Shot-2018-04-10-at-16.32.47.png" alt="" width="598" height="396" class="alignnone size-full wp-image-226457" /
Ashura Nassoro mshindi wa bodaboda kupitia shindano la ShikaNdinga2018 Daresalaaam akionyesha uwezo na kuthibitisha ushindi wake haukuwa wa kubahatisha.

Akizungumza wakati wakukabidhi zawadi za Washindi hao Meneja Mkuu wa Radio Efm na Tv E, Dennis Busulwa(Sebo) amesema kuwa washindi hao wameshinda pikipiki na kupatiwa tiketi ya kushiriki fainali za la shika ndinga zitakazo fanyika Dar es Salaam mara baada ya kuwapata washindi wa mikoani.

Kushoto Meneja Mkuu E-fm DennisSsebo akikabidhi kadi ya pikipiki kwa Ashura Nassoro ambae ni mshindi wa bodaboda upande wa wanawake.

Amesema kuwa siku ya jumatatu washindi hao watafika katika ofisi za Efm na Tv E kwa ajili ya kubadilisha majina ya kadi za pikipiki hizo kutoka jina la kampuni kwenda majina hao.

Washindi hao ambao wamepatikana kupitia mchakato mrefu ulioanza asubuhi kwa mbio z akukimbia na Vikombe vya maji kisha ikaja awamu ya pili ya kukimbia na mayai ambayo iliwapeleka fainali.

Katika hatua ya fainali ya kushika gari ndio iliyotia fora kwa wanawake kuweza kusimama kwa Zaidi ya saa moja wakti wanaume ndani ya nusu saa wanaume walikuwa washpata mshindo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents