Siku ya uchangiaji damu duniani, MeTL yatoa msaada wa vinywaji ofisi za damu salama (+Video)

Kuelekea siku ya uchangiaji damu duniani ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 1, 06, 2021  kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL) imetoa msaada wa vinywaji makao makuu kanda ya Mashariki kwaajili ya kuchangia kuwapatia wale ambao watachangia damu.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa vinywaji hivyo, Dkt Pendaeli Sifueli Meneja wa damu salama kanda ya Mashariki ambaye huudumia Mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro na Pwani amemshukuru Mo kwa mchango huo ambao utasaidia kuwapatia wale ambao watachangia damu.

”Leo hii tumepokea wageni ambapo wamekuja kutusaidia kama vile ambavyo tumewaomba, ili waweze kusaidia katika zoezi zima la uhamasishaji siku ya kuchangia damu duniani ambayo itaanza tarehe 1 – 14. Mwaka huu tumejikita kwenye kutoa elimu kwa vijana, kwani vijana ni dhamana ya taifa na kuhakikisha kuwa damu inapatikana.”

Kwa upande wake Afisa Mhamasishaji Jamii wa mpango wa Taifa wa damu salama, Marim Juma amesema baada ya kupokea mchango huo wanaimani kuwa kila ambaye atahitaji kupata kinywaji atapatiwa huku akiwaomba wadau wengine kujitolea kwakuwa mpango wa damu salamu ni zoezi ambalo lipo kila siku.

”Tuendelee kuwaomba wadau wengine, kwasababu mpango wa taifa wa damu salama unafanya kazi kila siku, kwa hiyo tuendelee kuwaomba wadau wengine watakao guswa basi tuendelee kuwasaidia wahitaji wa damu.”

Naye Afisa Mawasiliano MeTL, Nasra Ally amesema kuwa wamewapatia vinywaji hivyo ili kuwarahisishia zoezi lao la siku ya mchangiaji damu salama duniani. ”Tunayo furaha ya kualikwa katika mpango wa kuchangia damu salama kanda ya Mashariki, kwa kuja kutoa maji pamoja na juisi ambazo walituomba sisi kama wadau wakubwa wa zoezi la uchangiaji wa damu, tumekuwa nao kwa muda mrefu kwahiyo walikuwa na uhitaji kutoka kwetu kwaajili ya kuwapatia vinywaji hivyo ili iwe rahisi kwenda kwenye safari yao ya siku ya damu salama duniani.”

Related Articles

Back to top button