Michezo

Singida United wapewa elimu na SportPesa kuhusu mitandao ya kijamii (Picha+video)

Klabu ya Singida United leo jumatatu imetembelea Ofisi za makao makuu ya Kampuni ya SportPesa jijini Dar es salaam ambapo timu hiyo imepata mapokezi kwa semina fupi kuhusu mitandao ya kijamii.

Kwenye semina hiyo iliyoongozwa na Viongozi wa SportPesa wachezaji wameombwa kutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii ili kujitangaza zaidi na kufanya biashara nje ya soka.

Kwenye semina hiyo wachezaji wa Sportpesa wameshauriwa kujiongeza kwa kuwaonesha mashabiki wao vitu vyao binafsi kama video na picha wakiwa kwenye mazoezi na kujibu baadhi ya maoni ya mashabiki wao.

Mbali na hayo SportPesa pia wameelezea faida za mchezaji wa mpira wa miguu kujitangaza kuwa itamsaidia kutafutwa na makampuni makubwa ya vifaa vya michezo yeye kama yeye. Mfano Nike, Reebok, Puma n.k .

SOMA ZAIDI- Hivi ndivyo unavyoweza kushinda tiketi na SportPesa ya kwenda Uingereza kushuhudia mechi za EPL

Akizungumza baada ya semina hiyo mshambuliaji wa Singida United, Mkongwe Nizar Khalfan amesema Semina hiyo imekuwa ya muhimu kwake kwani awali alikuwa anachukulia kawaida mitandao ya kijamii huku akiwataka wachezaji wengine wa klabu za ligi kuu kujiunga kwenye mitandao ya kijamii.

Tazama picha na video za tukio hilo.

Uongozi wa SportPesa na Klabu ya Singida United.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents