Habari

Sio mimi wala Lissu tuliozuia ndege, serikali ilikuwa inadaiwa sisi tulihoji – Mh. Zitto

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa sio yeye wala Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu waliozuiwa ndege aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada isikamatwe.

Mh. Zitto amesema kuwa serikali ilikuwa inadaiwa hivyo wao walihoji tu na kuuliza maswali na hiyo ndiyo kazi yao kama upinzani kuendelea kuhoji.

Sio mimi wala ndugu Tundu Lissu tuliozuia ndege hii. Serikali ilikuwa inadaiwa na sisi tulihoji tu na kuuliza maswali. Ndio kazi yetu hiyo kama opposition na tutaendelea kuhoji. Mf. Nimeambiwa Serikali imelipa $63m kuokoa Hii ndege iliyokuja. Ndege mpya ni $31m. Tutahoji tu,” ameandika Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Ndege iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikuja Tanzania Marchi 30 ikitokea Canada ilipokuwa imeshikiliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents