Burudani

Soggy Doggy adai mashabiki wa sasa wanapenda ‘kutazama kuliko kusikiliza’

Rapper mkongwe na mtangazaji wa redio, Soggy Doggy amesema wimbo wake ‘Nafunga Zipu’ ulishindwa kufanya vizuri kwakuwa ulikosa video.

soggy dogy

Soggy ameiambia Bongo5 kuwa mashabiki wa sasa wanapenda kuangalia kuliko kusikiliza.

“Kwetu Studio ndio walikuwa na kazi yetu lakini baada ya kupata matatizo ya kuibiwa vifaa vyao vya studio, wakawa wameibiwa na material ya kazi yetu, tukakosa muda tena wa kukutana na kufanya video nyingine,” amesema Soggy kuhusu sababu ya kutotoka kwa video ya wimbo wake, Nafunga Zipu.

“G.Nako yupo busy, na wimbo bila video ni sawa na kazi bure kwa sasa. Kwahiyo ngoma ilikuwa kali ila ilikosa video ndio maana unaona hivyo. Lakini ilipata airplay kwenye redio ya kutosha hasa hasa mikoani, so kama tungepata video ngoma ingekuwa mbali zaidi. Lakini sasa hivi najipanga upya baada ya mwezi mmoja nitaachia ngoma mpya kali pamoja na video ili kuendeleza pale nilipoishia,” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents