Habari

Sony Music Entertainment kwenda Kenya kusaini wasanii

Sony Music Entertainment Africa inatarajia kwenda nchini Kenya. Lengo la ziara hiyo kwa mujibu wa vyanzo ni kwenda kutafuta wasanii (waliofanikiwa tayari) ili kuwapa mikataba na label hiyo itakayodumu kwa miaka mitano.

Tayari Sony wameshamteua mtu wa kupendekeza wasanii wa kula shavu kwenye kampuni hiyo kubwa duniani japo mkataba bado haujasainiwa.

Hivi karibuni kampuni hiyo ilimsainisha rapper wa kike wa nchini humo Xtatic, kwa mkataba wa kurekodi naye albam kadhaa na kusimamia kazi zake.

Mkataba huo ulimfanya Xtatic aliyezaliwa kwa jina la Gloria Edna Mecheo kuwa mkenya wa kwanza kuwa chini kampuni hiyo.

Kutokana na mkataba huo, Xtatic aliungana na wasanii wakubwa kama  Usher, Chris Brown, R Kelly na Pink walio chini ya Sony Music Entertainment.

Tuombe Mungu waje na Tanzania. Rose Muhando ndio msanii pekee nchini kuwa chini ya kampuni hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents