Burudani

Squeezer: Nilikuwa kimya kwa sababu za kifamilia

Rapper Squeezer amewataka mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kuwa hatokaa kimya kwa muda mrefu tena.

squeezer1

Akiongea na show ya Planet Bongo ya East Africa Radio, rapper huyo mwenye sauti nzito amesema sababu iliyomweka pembeni kwa muda ni kuweka sawa mambo ya kifamilia ambapo kaka kaka mkubwa alikuwa busy baada ya msiba wa baba yake.

“Bahati mbaya nilipata tatizo kwa kufiwa na baba yangu kwahiyo nisingeweza kuendeleza program zangu. Nilitakiwa kufanya vitu vingi hasa vya kifamilia na mimi ndio mtoto mkubwa halafu wa kiume na msiba ulikuwa Mbeya,” alisema.

“Kwahiyo nimejikuta mara nyingi na kuwa nasafiri sana kuweka mambo sawa ya kifamilia na kufuatilia. Lakini sasa hivi sitokaa kimya sana, mashabiki wangu watapata kazi zangu,” alisisitiza.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents