Bongo Movie

Steve Nyerere azungumzia tuhuma za kutumia cheo vibaya kuwanyonya wasanii wenzake

Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steve Nyerere amezungumzia madai ya kuwa anatumia vibaya madaraka na kuwanyonya wasanii wenzie sababu iliyofanya aliyekuwa katibu mkuu, William Mtitu ajiuzulu wadhifa wake.

Mwenekiti wa bongomovie Steve Nyerere

Akizungumza na Bongo5 leo, Steve amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii wa umoja huo wamekuwa wakimuonea wivu.

“Kwenye akaunti ya bongo movie kuna hela? Kwamba kiongozi aliyepita aliacha milioni 150! wewe umeacha zero point zero unazungumazia pesa hipi? huyo Irene Paul mimi siwezi shindana naye. Katika Maisha sishindani na mwanamke, hapa nilipofikia siwezi nikasimama na kujibishana na Irene Paul kwa hadhi niliyokuwa nayo katika nchi hii,” amesema Steve. Bongo movie ipo na itaendelea kuwepo na kuna mambo mazuri yanakuja, tena makubwa zaidi ya hayo. Kiongozi thabiti ni yule ambaye hajihudhuru na amechaguliwa na mwananchi. Mimi sijachaguliwa na mtu mmoja kwamba utakuwa, mimi nimechaguliwa na wanachama, kwahiyo kama wanachama wote wananihitaji mimi watasema. Kama wanachama wangekuwa mimi hawaniitaji ningekuwa nimeshaondoka na mimi kama kimbilio lao wamenichagua siwezi kujiudhuru! Na hiyo akaunti ya bongo movie ina shilingi ngapi? Hakuna kitu ni uroho wa watu wachache, hao ni wasanii wachache wenye wivu wa maendeleo, ni wivu wa vitu vidogo ambavyo ni vya kibinadamu,” ameongeza.

Mtitu alieleza sababu za kujiudhuru wadhifa wake kupitia Instagram.

mtitu

“Kwa kulinda heshima yangu binafsi nayakampuni yangu nimeona mimi kama MTITU nijivue rasmi leo nafasi ya uongozi na nitabaki kuwa kama mwanachama wa kawaida wa CLUB ya bongo movie sababu kiukweli SIPENDEZWI kwa asilimia kubwa na jinsi club inavyoendeshwa na sioni kama tunaelekea popote badala yake club imekuwa ni sehemu ya baadhi yetu kujipatia mkate wa kila siku kwa kutumia JINA LA CLUB …kitu ambacho SIKUBALIANi NACHO. Na ikumbukwe sina ugomvi wala chuki na mtu yeyote ndani ya bongo movie…. Wacha maisha yaendelea kama zamani..Nawatakia wèek end njema,” aliandika Mtitu kupitia Instagram.

Kwa upande Irene Paul aliiambia Take One ya Clouds TV kuwa uongozi huo wa juu wa Bongo Movie Unity umeoza.

“Kuna baadhi ya watu wanaamini bila wao bongo movies isingekuwepo, wanafanya bongo movie ni yao na wameishika, lakini tuulizane amefanya nini katika bongo movie ama hizo filamu anazofanya? Lakini mimi ndo mwanachama wa bongomovie leo hii naongea kwamba hakuna kitu nilichonufaika kupitia bongomovie. Silaumu viongozi wote, nazungumzia wale ‘big five’ wale watano wa mwazo, kuanzia rais mpaka mpaka cheo cha tano kutoka kwa rais. Sasa sijasema hawa wote wameoza ila katika haya ninakubali kuwa sikubaliani wa uongozi wao binafsi, especially ninaposema sikubaliani na uongozi binafsi ni sawa sawa na mtu aseme kwamba sikubaliani na uongozi wa Tanzania atakuwa anamkataa nani? simple!” alisema Irene Paul.

Irene-Bahati-Paul-cut
Irene Paul

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents