Habari

Sudan kuruhusu unywaji pombe kwa wasiokuwa waislamu

Waziri wa sheria wa Sudan Nasredeen Abdulbari, jana jioni amesema kuwa serikali ya nchi hiyo itaruhusu watu wasiokuwa waislamu kunywa pombe na kuimarisha haki za wanawake ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku ukeketaji wa wanawake katika hatua ya mabadiliko takriban miongo minne ya sera za misimamo mikali ya kiislamu.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takriban asilimia 3 ya idadi ya watu wa Sudan sio waislamu.

Vinywaji vya vileo vilikuwa vimepigwa marufuku tangu aliyekuwa rais Jaafar Nimeiri kuanzisha sheria ya kiislamu ya mwaka 1983 na kutupa chupa za pombe katika mto Nile katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Abdulbari amekiambia kituo cha televisheni cha kitaifa kwamba watu wasiokuwa waislamu hawatashtakiwa tena kwa kunywa pombe faraghani lakini marufuku hiyo bado inatekelezwa dhidi ya waislamu.

Serikali ya mpito iliyochukuwa mamlaka nchini humo baada ya kuondolewa kwa Omar al-Bashir mwaka jana, imeapa kuiongoza Sudan katika demokrasia na kutamatisha ubaguzi na pia kutafuta amani kati yake na waasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents