Habari

TACAIDS yadai mastaa wapo kwenye hatari zaidi ya kuathirika na virusi vya Ukimwi (Video)

Wakati dunia leo inaadhimisha siku ya Ukimwi duniani, December 1, Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini, (TACAIDS) imesema watu maarufu wakiwemo wasanii ni watu walio kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na ushawishi wao na hivyo wanatakiwa kupewa elimu.

Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho
Mwenyekiti wa TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho

Akizungumza na taasisi ya Global Shapers Community Dar es Salaam, Mwenyekiti TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho, alisema ushawishi wa wasanii hao unawafanya watamaniwe na watu wengi hali inayowaweka kwenye hatari.

“Watu wa muziki na burudani ni watu wenye ushawishi mkubwa sana,” alisema. “Wao wenyewe wapate elimu ili wajikinge kwanza halafu watoe ujumbe kwa sababu wanafuatwa sana. Ni watu ambao wana mvuto sio tu kwa vijana hata mimi ni watu ambao nawapenda sana kwenye muziki. Kwahiyo ningependa kuwasikia na wazungumze masuala ya Ukimwi,” alisisitiza Bi Fatma.

Pia alisema anavutiwa na utunzi na juhudi za wasanii mbalimbali wakiwemo Diamond Platnumz, Alikiba na Lady Jay Dee

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents