Afya

TAFITI: Wanaume wenye upara wapo katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo

Imeelezwa kuwa Wanaume walio chini ya miaka 40 ambao wanaupara kichwani na wale wenye nywele za rangi ya kijivu wako katika hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa ya moyo, hii ni kwa mujibu wa utafiti.

Picha inayohusiana

Utafiti huo uliofanywa na Idara ya Magonjwa ya Moyo barani Ulaya ( U.N. Mehta Institute of Cardiology) na Watafiti wengine wa Magonjwa ya Moyo kutoka India,  Ulifanywa kwa vijana 2000 kutoka nchini India ambapo ulionyesha kuwa wengi wao waliokuwa na ugonjwa wa moyo walikuwa na upara na nywele za kijivu ikilinganishwa na wanaume walio na nywele kichwani.

Dkt. Kamal Sharma mkuu wa Idara hiyo ya Magonjwa ya Moyo amesema watu wenye upara na wale wenye nywele za kijivu ambao wapo chini ya miaka 40 wapo hatarini mara 5 ya watu wenye nywele kichwani.

Kwa majibu ya Utafiti wetu unasema kuwa miongoni mwa wanaume wenye upara na nywele za kijivu wapo katika hatari ya kupatwa na matatizo ya magonjwa ya moyo mara tano zaidi nya wale wenywe nywele lakini hii haiwezi kuwa ni sababu ya magonjwa ya moyo kwani bado ongezeko la mafuta mwilini ni sababu kubwa inayochangia magonjwa ya moyo.“amesema Dkt. Sharma kwenye mahojiano yake na mtandao wa Medical News Today.

Utafiti huo wa Idara ya Magonjwa ya Moyo barani Ulaya ( U.N. Mehta Institute of Cardiology) utasomwa katika kongamano la 65 la kila mwaka la magonjwa ya moyo nchini India.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents