Habari

TEF lataka waliojeruhiwa kwenye ajali ya moto mkoani Morogoro washitakiwe, Ladai walikuwa ni waporaji

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kushtushwa na taarifa za vifo vya Watanzania 69 walioungua kwa moto wakati wakichota mafuta kutoka katika Lori lililopinduka eneo la Msamvu Mjini Morogoro, jana Agosti 10, 2019 huku jukwaa hilo likitaka waliojeruhiwa washtakiwa pindi watakapopona majeraha yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deodatus Balile imesema kuwa vifo hivyo vimetokana na tabia iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuchukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali.

Tumeshuhudia picha za watu waliofariki kwa kuungua moto zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na upashanaji habari. Tunakemea tabia hii na kuitaka jamii iache mara moja tabia hii ya kinyama isiyo ya utu,” amesema Balile kwenye taarifa hiyo.

Kuhusu majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo, Balile amesema majeruhi hao wakipona washtakiwe ili wajiepushe na tabia
ya uporaji.

Ikilazimu, wote watakaopona katika ajali hii washitakiwe kwa mujibu wa sheria, ili iwe fundisho kwao na wengine kuwa ikitokea ajali tunapaswa kusaidia majeruhi na kuokoa mali zao badala ya kupora.” amesema Balile na kuongeza kuwa “Tunaomba viongozi wa dini, wazazi, viongozi wa kisiasa na jamii kwa ujumla itumie ajali hii kufundisha watoto na vijana maadili mema ya kuwa watu wa msaada mtu anapopata ajali kwa kusaidia majeruhi na kuokoa mali za waliopata ajali badala ya kuwapora,”.

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents