Habari

Tenga atoa sababu ya kutogombea tena urais wa TFF

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amesema hawezi kugombea tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo unaotarajia kufanyika February 24 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Tenga amesema wakati anaingia madarakani miaka minne iliyopita alikuwa na kazi ya kufanya, ambayo ilikuwa ni kujenga taasisi ya soka nchini, na kwamba hawezi kuendelea tena kwani uongozi ni kijiti na kwamba huu sasa wakati wa kukimbizwa na mtu mwingine.

“Nimekaa madarakani kwa miaka minane kwakweli ni miaka mingi sana,tangu mwaka 2004 ambapo wakati huu kulikuwa na ajenda maalum ya kuleta mabadiliko ya msingi katika soka”alisema Tenga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents