TETESI: Mauricio Pochettino kurithi mikoba ya Conte, Chelsea
Ikiwa ligi kuu nchini Uingereza tayari imefikia tamati kubwa ni hekaheka za usajili ambapo kwa hivi sasa kocha wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino anahusishwa kutua Chelsea ili kurithi mikoba ya Antonio Conte ambaye anatarajiwa kuondoka mara baada ya mchezo wake wa mwisho wa fainali ya FA atakapo wakabili Manchester United siku ya Jumamosi.
Chelsea imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao na hivyo Muitalia huyo kuondoka Stamford Bridge ikiwa imepita miezi 12 tu toka akipatie ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kikosi hicho cha The Blues.
Chini ya Pochettino, Spurs imefanikiwa kufuzu michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa miaka mitatu mfululizo huku ikiwa inatumia bajeti ndogo ya fedha ukilinganisha na timu kama Manchester City, Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal.