Videos

Trailer: ‘Going Bongo’ filamu ya Kimarekani iliyofanyika Dar es Salaam (Bonge la Movie)

Going Bongo ni filamu ya Kimarekani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Inatarajiwa kuwa filamu bora kabisa kuwahi kufanyika Tanzania na hata Afrika Mashariki kwa ujumla.

Going Bongo ni filamu inayomhusu daktari (Dr.Lewis Burger) wa Kimarekani (nafasi imechezwa na Ernest Napoleon) ambaye anajitolea kimakosa kuja Tanzania kwa mwezi mzima. Filamu hii imeshutiwa Dar-es-Salaam na Los Angeles, California.

Pamoja na kuwa na waigizaji wengine wengi wa Marekani, filamu hiyo imeshirikisha pia waigizaji wa Tanzania wakiwemo Sauda Simba Kilumanga, Evans Bukuku, Mzee Chilo na Amby Lusekelo.

Wimbo wa Ngwair, Nipeni Deal umetumika kwenye video hii.

http://youtu.be/gHoOJ990-DA

Filamu imeandikwa na kutayarishwa na Ernest Napoleon na itatoka December 12 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents