Habari

Trump akataa ndege mpya ya Air Force One

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amepanga kufuta bajeti ya ununuzi wa ndege mpya ya Air Force One ambayo hutumiwa na marais wa nchi hiyo.

maxresdefault

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Trump ameandika, “Boeing is building a brand new 747 Air Force One for future presidents, but costs are out of control, more than $4 billion. Cancel order!.”

Serikali ya Marekani iliingia mkataba na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing kwa ajili ya kutengeneza ndege mbili mpya ambazo zitawabeba marais wa nchi hiyo pamoja na viongozi wengine.

Ndege hizo zinatarajia kukamilika mwaka 2024.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents