Tufanye haya ili kukuza na kustawisha sekta ya mawasiliano Tanzania

Tanzania imepata mabadiliko makubwa ya teknolojia katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Leo hii, Tanzania ina watu zaidi ya milioni 11 wanaotumia mtandao wa intaneti kupitia simu zao za mkononi.

Maendeleo haya ni fursa ya kubadili maisha na kukuza maendeleo ya mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Moja ya wadau wakubwa katika kuleta mabadiliko hayo yenye tija kubwa kwetu ni makampuni ya simu ambayo yamekuwa yakishirikiana na serikali kwenye ubunifu mbalimbali mfano mmojawapo ukiwa ule mfumo wa kusajili vizazi na vifo, mfumo ambao umesaidia watoto wengi nchini kupata vyeti vya kuzaliwa haraka.

Sote tunajua umuhimu wa cheti cha kuzaliwa sio tu Tanzania bali dunia nzima pale unapotaka vitu kama chanjo, vitambulisho, pasi za kusafiria, ajira na kadhalika.

Tigo Tanzania inajulikana kama kampuni ambayo imewezesha jambo hili la usajili ambalo limewezesha wazazi kusajili na kupata vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao kwa haraka zaidi.Umoja huu kati ya serikali na kampuni ya Tigo Tanzania katika kutengeneza kitu ambacho kinatatua changamoto za wananchi ni mfano bora namna gani uwekezaji wa kimkakati na ushirikiano unaweza kukuza maendeleo yetu.

Ili kuhakikisha kwamba kizazi hiki na kijacho vinanufaika na ukuaji wa teknolojia na matunda yake lazima sisi kama nchi tuendelee kujenga mazingira ya uwekezaji katika teknolojia na kampuni za simu na kushirikiana nazo.

Mazingira mazuri ya kuwekeza ni pamoja na sera bora zilizopimwa na kuundwa vizuri kwa ajili ya sasa na siku zijazo.

Katika kufanya hivyo sisi kama taifa tutakuwa tumehakikisha sekta ya mawasiliano ya simu inakua na kuvutia mitaji mikubwa ambayo ni muhimu kwani sekta hii huhitaji uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu.

Matokeo yake ni wananchi na nchi yetu kuvuna faida zaidi kiuchumi na kijamii kutokana na kupanuka na kukua kwa teknolojia na mawasiliano.

Related Articles

Back to top button