Burudani

Tunajifunza nini kutokana na Alicia Keys, Swizz Beatz na Drake kuizimia Ojuelegba ya Wizkid?

Wizkid ni msanii wa Nigeria mwenye connection nyingi kwa sasa pengine kuliko msanii mwingine yeyote anayeishi barani Afrika.

Wizkid n breezy

Muimbaji huyo tayari ameshafanya collabo na wasanii wakubwa wa Marekani akiwemo Chris Brown ambaye mwaka jana walitumbuiza pamoja wimbo wao African Bad Girl nchini Afrika Kusini. Msanii huyo alidai kumwandikia nyimbo Rihanna.

“Nilienda studio kuandika kitu kwaajili yake [Rihanna], alikuwepo studio pia, big shout kwa Rihanna,” Wizkid alisema kwenye mahojiano ya mwaka jana. “Hivyo tulitengeneza kitu pamoja na naamini itachukuliwa. Tutaendelea kufanya vitu pamoja, unajua ni mtu mzuri. Naenda tena Los Angeles na bila shaka ntaingia tena studio naye,” aliongeza.

Mwaka huu nadhani umekuwa wa mafanikio zaidi kwa staa huyo. Wimbo wake Ojuelegba umekuwa na mafanikio makubwa kwake. Wimbo huu licha ya watu wengi kutouelewa unamaanisha nini, umeendelea kupenya na hadi sasa wasanii wengi wa Marekani wameukubali akiwemo Drake ambaye aliamua kuweka verse yake kwenye remix ya wimbo huo.

Drake aliufahamu wimbo huo kupitia rapper wa Uingereza, Skepta aliyemsikilizisha na akaupenda.

Habari njema zaidi na ambayo inadhihirisha ukubwa wa Wizkid kwa sasa ni pale wanandoa, producer Swizz Beatz na mke wake, Alicia Keys kupost wote video wakiucheza wimbo huo kwa furaha.

Alicia Keys alipost video Instagram akiwa amevalia nguo ya dhambarau akicheza wimbo huo na kuandika ‘wimbo huu hunifanya niwe na furaha’ na kumtag Wizkid. Swizz naye alipost kipande cha video akiufurahia wimbo huo na kuandika, ‘mmoja wa wasanii ninaowapenda kwa sasa, Wizkid, Good Vibes.’

Kabla ya hapo Swizz alipost kava la album ya Wizkid ‘Ayo’, na pia Alicia kupost video nyingine wakicheza na mume wake huyo wimbo mwingine uliopo kwenye album hiyo, Carol. Swizz Beatz na Alicia wiki hii wanaadhimisha miaka mitano ya ndoa yao na hivyo wapo likizo.

Tunajifunza nini kutokana na hilo?

La kwanza ni kuwa milango ya Marekani kwa muziki wa Afrika huenda ikaanza kufunguka taratibu. Sio jambo rahisi lakini kama watu muhimu kwenye industry kama hao wameupenda wimbo huo wasiouelewa hata unamaanisha nini, inatia moyo kuwa kumbe muziki wa Afrika unaweza kufika sehemu.

Pili, tumepata uthibitisho wa ule ukweli kuwa lugha kwenye muziki si kitu cha kumzuia mtu kuupenda wimbo. Nguvu ya wimbo ipo kwenye melody na mdundo wake tu.

Tatu, nimegundua kuwa ‘huenda’ Wamarekani wameanza kuchoka kusikia ladha za muziki zile zile walizozizoea na sasa wanataka kusikiliza muziki mpya. Muziki wa Afrika pengine ni chaguo lao sahihi kwa sasa pale wanapotaka kusikia ladha tofauti. Wizkid awe mfano kwa wasanii wengine kuwa waendelee kutengeneza muziki mzuri wenye ladha ya kiafrika kama wanataka kuwashika wamarekani pia.

Nne, Wizkid ni Akon wa pili. Muda si mrefu Wizkid linaweza kuwa jina kubwa Marekani. Hakuna shaka kuwa label kubwa za Marekani zitafikiria kumsaini ili kumuingiza kwenye industry ya Marekani. Mashavu aliyopewa na Drake, Alicia Keys na Swizz Beatz ni makubwa mno!

Una lipi ulilojifunza pia? Tufahamishe hapo chini tafadhali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents