Michezo

Ubabe uwanjani waiponza Spurs na West Ham

Klabu ya West Ham na Tottenham za nchini Uingereza zimeadhibiwa na chama cha soka ‘FA’ kwa kitendo cha wachezaji wao kuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo wao wa derby uliyowakutanisha wababe hao siku ya Jumamosi katika jiji la London.

Katika mchezo huo ambao uligubikwa na vurugu dakika ya 95 kwa baadhi ya wachezaji wa pande zote mbili kutoelewana baada ya muamuzi, Michael Oliver kuipatia Spurs ‘free-kick’  kutokana na makosa yaliyojitokeza kwa mchezaji wa West Ham, Andy Carroll dhidi ya Fernando Llorente.

Wachezaji, Carroll, Llorente, Winston Reid na Eric Dier wamehusishwa katika vurugu hizo na hivyo timu zao zitapaswa kuwa na majibu yakueleza mbele ya FA.

Taarifa kutoka FA zinasema kuwa “West Ham United na Tottenham Hotspur wameshtakiwa kufuatia vurugu zilizotokea katika mchezo wao wa Septemba 23 siku ya Jumamosi.

Klabu hizo sasa zitatakiwa kujibu mashtaka yanayowakabili hapo kesho siku ya Alhamisi Septemba 28.

Katika mchezo huo Spurs iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 2.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents