Vijana wa Kariakoo, Mabingwa wa Nchi Simba Sports Club kukabidhiwa kombe lao Julai 8, 2020 mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetoa taarifa hiyo hii leo.
”Baada ya Simba SC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2019/2020, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inawataarifu kuwa sherehe za kukabidhi kombe kwa timu hiyo zitafanyika mjini Ruangwa mkoani Lindi Julai 8, 20220.” – Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
”Shughuli hiyo itafanyika kwenye uwanja wa wa Majaliwa mara baada ya kumalizika kwa mchezo namba 340 wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Namungo FC na Simba SC.”