HabariSiasa

Ufaransa kuchunguza ajali ya shirika la ndege la Yemen ya mwaka 2009 

Mahakama nchini Ufaransa inatarajiwa kuaanza kusikiliza kesi inayohusu kuanguka kwa ndege ya shirika la ndege la Yemen ya mwaka wa 2009 ajali iliyosababisha vifo vya watu 152.

Uchunguzi wa mahakama unakuja wakati waakilishi wa shirika hilo la ndege wakikosa kujiwasilisha katika  mahakama hiyo  wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Yemen.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa kipindi cha wiki nne na iwapo watakutwa na kosa watatozwa faini ya euro 225,000 kwa kusababisha mauaji na majeraha kwa binadamu.

Tarehe 29 ya Mwezi Juni mwaka wa 2009 ndege hiyo aina ya Yemenia 626 ilikuwa inakaribia  jiji kuu la visiwa vya la Comoros, Moroni eneo jirani na taifa la Msumbiji na Madagascar kabla ya kuanguka katika bahari Hindi.

Abiria wote waliokuwa wameabiri ndege hiyo walifariki kwenye ajali hiyo isipokuwa Bahia Bakari,wakati huo akiwa mtoto mwenye   umri wa miaka 12.

Kati ya abiria 142 waliokuwa kwenye chombo hicho walikuwa wahudumu 11 wa ndege hiyo na raia 66 wa ufaransa waliokuwa wahehamishwa katika uwanja wa ndege wa Sanaa wakati huo.

Bakari Bahia katika kitabu chake alichokiaandika anaeleza yaliomkumba baada ya ajali hiyo kabala ya kuokolewa siku ifuatayo baada yake kuwa  baharini kwa saa kumi na moja.

Ufaransa ilituhumu mamlaka nchini Comoros kwa kuchelewesha uchunguzi wa kubaini chanzo cha ajali hiyo familia za waathiriwa nazo zikihituhumu Yemen kwa kupanga kuhujumu uchunguzi dhidi ya shirika lake la ndege.

Kesi hiyo inaanza kusikizwa baada ya miaka 13 ya kusubiri haki japokuwa wachunguzi na wataalam wa mambo ya usafiri wa angani  walibaini kuwa ndege hiyo haikuwa na changamoto zozote za  kiufundi ila wahudumu wake walikosea wakati ndege hiyo ilipokuwa inatarajia kutua jijini Moroni kabala ya chombo hicho kupoteza mwelekeo.

Karibia watu 560 wamejumishwa katika orodha ya walalamishi wengi wao wakitokea mjini Marseille kusini mwa Ufaransa nyumbani kwa wengi watu walioathrika na ajali hiyo ya mwaka wa 2009.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents