Ujerumani yatoa tahadhari ya kimbunga Sabine
Kimbuka cha msimu wa baridi, ambacho kimepewa jina la Sabine nchini Ujerumani, na ambacho awali kilitabiriwa kuvikumba Visiwa vya Uingereza kwa sasa kinatarajiwa kuelekea Kaskazini mwa Ulaya.
Mamlaka imeonya kwamba upepo mkali ambao utatokea Bahari ya Atlantik, utasababisha kimbunga kitakachovuma kwa nguvu ya kilometa 120 kwa saa, mvua kali na mvua zenye ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo ya bara Ulaya.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha DW, Idara ya hali ya hewa ya Ujerumani DWD imesema kimbunga Sabine kinatarajiwa kupiga Kaskazini/Magharibi mwa Ujerumani nyakati za asubuhi ya leo, na kisha kuelekea Kusini mwa Ujerumani na hasa katika jimbo la Bavaria.
It will be a very wet and windy start to #Sunday as #StormCiara starts to cross the UK. Several #WeatherWarnings are in force ⚠️⚠️⚠️⚠️
Stay safe and keep #WeatherAware pic.twitter.com/PwgcNn1qlQ
— Met Office (@metoffice) February 8, 2020
Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa limesema abiria wajiandae na matukio ya kusitishwa kwa safari za ndege.