Habari

Ulaya wataka majibu madai ya upelelezi wa Marekani 

Mataifa kadhaa ya Ulaya yametaka kupatiwa majibu kufuatia ripoti kuwa Marekani iliwapeleleza wanasiasa wa nchi hizo washirika kwa kutumia miundombinu ya mawasiliano ya Denmark kati ya mwaka 2012 hadi 2014.

Deutschland Frankreich PK Ministerrat | Merkel und Macron

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wamesema kwa pamoja kuwa kuendesha ujasusi miongoni mwa mataifa washirika ni jambo lisilokubalika na kuwa wanataraji kupata ufafanuzi kutoka Washington na Copenhagen.

Hayo yanafuatia ripoti ya uchunguzi iliyorushwa siku ya Jumapili na vyombo vya habari barani Ulaya ambayo imefichua kuwa taasisi ya usalama wa taifa ya Marekani NSA ilitumia mifumo ya mawasiliano ya Denmark kuwapeleleza wanasiasa wa ngazi ya juu nchini wa Ufaransa, Ujerumani, Norway na Sweden.

NSA ilifanikiwa kudukua mawasiliano ya ujumbe mfupi, mazungumzo ya simu na hata matumizi ya intaneti ikiwemo ya kansela Angela Merkel wa Ujerumani na viongozi wengine wa serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents