Burudani

Update: Soundcity hamuwezi kututisha kwa lolote – Meneja wa P-Square awajibu!

Beef kati ya kituo cha runinga Soundcity TV ya Nigeria na kundi la P-Square inazidi kupamba moto.

Jude-Okoye

Meneja wa kundi la P-Sqaure ambaye pia ni kaka yao, Jude Okoye amekijibu kituo hicho kilichotoa maelezo ya kwanini hakioneshi video za P-Square (Ingia hapa).

Jude ametumia Twitter kuishutumu Soundcity kuwa haiwalipi wasanii mirahaba na wao hawalalamiki, hivyo wasidhani kuwa wanawasaidia wasanii kucheza video zao kwasababu wao (Soundcity) wanatengeneza mamilioni kwa kuonesha kazi za wasanii bure.

Jude ameandika:

“Kazi yangu ni kutengeneza videos na kazi ya Soundcity ni kuonesha videos.”

“kama ambavyo mna haki ya kuamua video za kucheza ndivyo na sisi tuna haki ya kuamua kutumbuiza bure ama laa.”

“Mnaweza kuendelea kuwatishia wasanii wengine lakini sio P-Square”.

“Vituo vingine vyenye sifa nzuri havina tatizo kuwalipa wasanii kwenye events zao”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents