Uraia wa Nchi mbili

Image
Suala la uraia wa nchi mbili “Dual Citizenship” ni jambo ambalo limekuwa likizungumziwa na wadau mbali mbali pamoja na serikali yetu kwa nyakati tofauti.

Suala hili ni moja ya mambo ambayo yanazipa tabu nchi nyingi ambazo kimtazamo wa haraka haraka ni zile zinazotumia lugha ya kiingereza. Kwa mfano tu nchi kama Zambia, Botswana, Uganda, Africa Kusini, Kenya, Zimbabwe na Tanzania yenyewe.

Kitu ambacho hakieleweki ni vipi wananchi wa nchi hizi ni tofauti na nchi nyingine za Africa Magharibi, Africa ya Kaskazini na baadhi ya nchi zilizo kusini mwa Africa kama Msumbiji na Angola zilivyoweza kuruhusu raia wake kuwa na uraia wa nchi mbili. Je suala hili limeathiriwa na mtazamo uliotokana na siasa za wakoloni waliotutawala? au uoga katika masuala ya maisha yenye tamaduni mchanganyiko?

Uwezekano wa kuwa na uraia wa nchi mbili unaweza kunufaisha taifa letu kwa kuwapa nafasi ya kuwekeza na kurudi nyumbani kuchangia maendeleo ya jamii kwa watanzania waliyopata uraia wa nchi nyingine kwa njia moja au nyingine.

Mfano mzuri ni Kali Ongala mtoto wa mwanamuziki nguli wa zamani Mzee Remmy Ongala, kijana huyu ambaye kwa sasa anasakata kabumbu nchini Sweden alizaliwa Tanzania huku mzazi mmojawapo akiwa Mwingereza.

Katika kulinda maslahi ya wanawe mama mzazi wa Kali Ongala aliamua kuwachukulia uraia wa Uingereza wanawe ili wapate faida ya kuwa na uraia wa nchi hiyo. Akiwa ni mmoja wa vijana waliokulia na kupata elimu yake ya msingi na sekondari Tanzania pamoja na kupata nafasi ya kujifunza na kucheza soka Tanzania hasahasa kwenye timu za Abajalo pale sinza na Yanga zote za Dar es Salaam.

Akiwa na mapenzi ya dhati na nia ya kuitumikia nchi aliyotumia muda mrefu wa maisha yake kKali Ongala alitakiwa kuukana uraia wa Uingereza ili aweze kuichezea timu ya Taifa Stars, kutokana na jambo hilo kuwa gumu kwa mchezaji huyo kukubali ilibidi atolewe kwenye timu ilipokuwa ikijiandaa kushiriki mashindano ya kuwania kufuzu kushiriki kombe la dunia.

Maswali ya muhimu kwa wasomaji wetu kujiuliza je ni watanzania wangapi wenye hali inayofanana na Kali Ongala? Na je ni kwa kiasi gani Tanzania inakosa huduma ya watu wenye moyo na uchungu wa kulitumikia taifa kwa kuwa tu ni lazima waukane uraia walionao kwa wakati huo? Tunasubiri maoni yenu wadau.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents