Habari

Urusi yaionya Marekani kisa mradi wa gesi

Serikali ya Urusi imesema Marekani haipaswi kuweka shinikizo kwa taifa lolote katika ridhaa juu ya kuidhinisha matumizi ya mradi wake wa bomba la gesi wa Nord Stream 2.

Mradi huo mpya uliokamilika unasubiri ridhaa ya Ujerumani, kabla ya kuanza kusafirisha gesi kupitia bomba hilo.

Marekani na baadhi ya mataifa ya Ulaya yanapinga bomba hilo, ambalo linapita kando ya Ukraine na kujengwa katika namna ya kusambaza gesi moja kwa moja kutoka Urusi hadi Ujerumani kupitia Bahari ya Baltic.

Wanasema hatua hiyo itaifanya Ulaya kuitegemea zaidi gesi ya Urusi, lakini baadhi ya serikali za mataifa ya Ulaya zinasema bomba hilo ni kiungo muhimu na salama katika usambazaji wa nishati hiyo kwa matifa yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents