Michezo

USAJILI: Deogratius Munishi (DIDA) apata timu Afrika Kusini

Mlindalango wa klabu ya Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania, Deogratius Munishi (Dida)  yuko nchini Afrika Kusini tangu wiki iliyopita kwaajili ya kupata timu ya kuichezea.

Golikipa wa klabu ya Yanga SC, Deogratius Munishi (Dida)

Golikipa huyo wa Yanga kwa sasa amejiunga na klabu ya Pretoria University kwa majaribio.

Dida, kabla ya kutimkia huko, alikuwa akinolewa na kituo cha makipa cha Tanzania Goalkeeping Training Center (TGTC) kinachomilikiwa na mlindalango wa zamani wa Taifa Stars na klabu za Yanga, Sigara na Mtibwa Sugar, Peter Manyika.

Mmiliki wa kituo hiko Manyika amethibitisha kuwepo Afrka Kusini kwa mchezaji huyo.

“Tumefanya naye mazoezi hapa kwa kipindi na alikuwa akijiandaa kwa ajili ya safari yake ya Afrika Kusini lakini hakutuambia anakwenda timu gani. Ameondoka yuko vizuri kaiva bila shaka atafanya vizuri na sisi tunamwombea mafanikio mema,” amesema Manyika.

Dida kabla ya kwenda Afrika Kusini aliutaarifu uongozi wa Yanga kuwa anakwenda kutafuta maisha huko lakini hakuweka wazi ni klabu ipi.

“Ameomba ruhusa ya kwenda Afrika Kusini kwaajili ya kutafuta maisha tukamruhusu moja kwa moja,” amesema Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa kwa msisitizo.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents