Burudani

USHAHIDI: Bora mniuwe, Tupac hajafa yupo Malaysia – Atoboa siri mtoto wa Suge Knight (+video)

Mtoto wa rapper nguli nchini Marekani, Suge Knight ajulikanaye kwa jina la Suge J. Knight ametoa ushahidi kuwa Tupac Shakur hajafa bado yupo hai, na stori zote zinazoandikwa kuwa alikufa ni za uongo kwani yupo nchini Malaysia  na mwenye afya njema.

tupac-suge

Suge J. Knight ameweka ushahidi huo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuonesha baadhi ya picha na meseji za Tupac, huku akimtaka 50 Cent naye aongee ukweli kuhusu kufichwa kwa Tupac.

Knight alianza kutoa ushahidi kupitia ukurasa wake wa Instgram, ambapo aliweka posti ya kwanza iliyokuwa na maneno yaiyosomeka  “Tupac is alive.” akimaanisha Tupac ni mzima.

https://www.instagram.com/p/BocV6_MnzFQ/?taken-by=sugejknight

Baada ya posti, aliombwa na wafuasi wake aoneshe ushahidi na yeye akaamua kuweka posti nyingine iliyokuwa na Meseji (iMessage) akionywa na watu aliowaita Illuminati wakimtaka aachane na taarifa hizo la sivyo watampoteza.

“Unaongea sana, huu ni muda wako kuondoka” naye akawajibu “Ukweli utajulikana na siendi popote pale”.

https://www.instagram.com/p/Bocs2UlnbF_/?taken-by=sugejknight

Baada ya mkwara huo, Knight aliendelea kuposti picha na mara hii aliposti picha ya Tupac akiwa na 50 na nyingine akiwa na Beyonce na kuandika “5O Cent ongea kila mtu anaona, Tupac hajafa najua watanipoteza na mimi ila sijali“.

https://www.instagram.com/p/Boc85pUHUzw/?taken-by=sugejknight

https://www.instagram.com/p/BodLsx8HWrJ/?taken-by=sugejknight

Baada ya kuona haeleweki akaamua kuposti video kwenye Insta Story akidai kuwa Tupac yupo hai na mzima wa afya na anaishi nchini Malaysia.

https://www.instagram.com/p/BodWhBknnK8/?taken-by=sugejknight

Knight aliendelea kusisitiza kuwa Illuminati wanalengo la kupoteza watu wote wanaoonekana kuwa na ushawishi mkubwa na akisistiza kuwa ameongea hayo akiwa mzima kiakili yaani hajatumia madawa.

https://www.instagram.com/p/BodWhBknnK8/?taken-by=sugejknight

https://www.instagram.com/p/Boe5ABeHCKP/?taken-by=sugejknight

Akaamua kuweka kabisa ushahidi wa picha na video za Tupac, huku akieleza kuwa ni picha za sasa hivi za Tupac akiwa nchini Malaysia , “Wanawadanganya nyie tu, huyu jamaa yupo hai”.

https://www.instagram.com/p/Boe-0ffHz2W/?taken-by=sugejknight

https://www.instagram.com/p/BoftCcdntkU/?taken-by=sugejknight

Hata hivyo, ameshambuliwa na baadhi ya watu wakimwambia kuwa anawatoa watu kwenye reli baada ya baba yake wiki hii kuhukumiwa kifungo cha miaka 28 jela kwa kosa la kugonga mtu na gari na kukimbia.

Baba yake, Suge Knight ambaye kwa sasa yupo jela, inatajwa kuwa alihusika kwa kiasi kikubwa kwenye mipango hiyo ya kifo cha Tupac.

Mnamo September 7, 1996, Shakur alipigwa risasi kadhaa akiwa barabarani huko Las Vegas, Nevada. Alikuwa akitoka kwenye pambano la ngumi kati ya Mike Tyson na Bruce Sheldon.

Mpaka sasa mamilioni ya watu ulimwenguni wanaamini kuwa Tupac aliuawa kwa kupigwa risasi, lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja juu ya kifo hicho.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 30 walidaiwa kulipwa kusaidia kudanganya kifo hicho wakiwemo polisi, madaktari na mashuhuda na mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kuongea.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents