Usiku wa visasi barani Ulaya Manchester City Vs Liverpool, AS Roma vs FC. Barcelona
Michuano ya Ligi ya mabingwa Barani Ulaya itaendelea tena usiku wa leo Aprili 10 kwa viwanja viwili kuwaka moto na huku wadau na wapenzi wa soka wakitaraji kushuhudia timu zilizofungwa mchezo wa awali zikilipa visasi.
Manchester City iliyokubali kichapo mujarabu cha mabao 3-0 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa awali uliyopigwa Anfield sasa itakuwa nyumbani uwanja wa Etihad huku ikiwa na kiuu ya kulipiza kisasi cha kufungwa na ikiwezekana kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Nyota wa Liverpool raia wa Misri, Mohammed Salah
Nyota wa Liverpool raia wa Misri, Mohammed Salah tayari amewasili kwenye uwanja wa mazoezi tayari kujiweka sawa kuwakabili City huku akiwa pamoja na wachezaji wengine akiwemo Sadio Mane ambaye hii leo anatimiza miaka 26.
This man turns 2️⃣6️⃣ today…
Hoping for a memorable birthday! 😄 pic.twitter.com/M5SE7f3Ptd
— Liverpool FC (@LFC) April 10, 2018
Meneja wa Liverpool, Klopp ameonekana kuwa bora zaidi ya Guardiola kwani rekodi zinaonyesha kuwa amemshinda mara saba kwenye michezo 13 waliyokutana na Mhispania huyo.
Wakati kwenye mchezo mwingine ni AS Roma iliyofungwa mabao 4 -1 dhidi ya FC. Barcelona itakuwa nyumbani kuwaalika wafalme hao wa soka wa Hispania huku wakihitaji kushinda goli nyingi zaidi ili kujihakikishia kusonga mbele.
Timu za Liverpool na Barcelona kama zitafanikiwa kupata ushindi au sare yoyote kwenye mchezo huo utako anza majira ya sa 3: 45 zitakuwa zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya.