Habari

Uturuki: Watu 29 wafariki katika tetemeko la ardhi, juhudi za uokoaji zaendelea

Juhudi za uokozi bado zinaendelea katika mji wa Elazig kufuatia tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8, cha Richter lilopiga Mashariki mwa Uturuki.

Image result for Uturuki Elazig 29 died

Kwa mujibuwa wa shirika la habari la DW, Watu wapatao 29 wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakiwa bado wamekwama chini ya vifusi vya majumba yaliyoporomoka, hayo ni kulingana na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Suleyman Soylu.

Waziri huyo ameongeza kwamba zaidi ya watu 15,000 wamekimbilia kwenye vituo vya muda vya kuwahifadhi watu ikiwa ni pamoja na kumbi za michezo na za vyuo vikuu.

Rescue workers search through the rubble in Elazig Saturday.

Watu wengine 5,000 wamejihifadhi katika mahema. Wengine wapatao 1,500 wamepelekwa hospitalini kwa matibabu huko mjini Elazig pamoja na miji mingine jirani. Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa ni wilaya ya Sivrice ya Elazig, lakini pia lilitikisa maeneo ya miji mengine ya karibu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents