Burudani

Vanessa Mdee kuachia album mwakani, itaitwa ‘Money Mondays’

Mshindi wa tuzo za AFRIMA 2014, kwenye kipengele cha Msanii bora wa kike Afrika Mashariki, Vanessa Mdee ataachia album yake ya kwanza mwakani. Muimbaji huyo wa ‘Hawajui’ amedai kuwa album hiyo itaitwa ‘Money Mondays’.

“Ni kwasababu Jumatatu kila mtu huamka na lengo la kutengeneza pesa,” alisema Vanessa kuhusu sababu za kuipa album yake jina hilo.

“Haijalishi kama unatengeneza nyingi au kidogo. Kule kujituma, kuhangaika ndio vitu hiyo album imebeba. Ni kuhusu kuhangaika na kupata kile unachotaka,” aliongeza.

Sikuwahi kuota kuwa ningekuwa hapa lakini nimethubutu kujaribu, kujipa changamoto mwenyewe, na leo tuko hapa tukiongea kuhusu Money Mondays.”

Hadi sasa muimbaji huyo ambaye jina lake la utani ni ‘Vee Money’, ameshatoa nyimbo nne, Closer, Come Over, Hawajui pamoja na Siri aliyoshirikiana na Barnaba.

Wiki hii pia akiwa pamoja na Barnaba, Aika, AVID na Nahreel waliachia video na wimbo uitwao ‘WCD’.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents