Burudani

Vanessa: Namuombea Jacky Patrick atoke jela mapema

Vanessa Mdee amesema anamuombea Jacky Patrick atoke jela mapema.

page

Jacky aliyefungwa jela nchini China baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aliwahi kuwa mpenzi wa Jux, ambaye kwa sasa ni boyfriend wa muimbaji huyo wa Niroge.

“Namuombea atoke jela mapema, nadhani matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo tunafiria sisi,” ameiambia Global TV.

“Sidhani hata kama huwa ananifikiria, nadhani anafikiria familia yake na hali ambayo anakosa maisha ya kawaida,” aliongeza.

Vanessa aliyeachia wimbo mpya Niroge hivi karibuni alisisitiza kuwa hakumuibia Jacky bwana (Jux) na kwamba alikuwa akimfahamu msichana huyo kama model wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents