Michezo

Beki wa Manchester City Martin Demichelis ashtakiwa kwa kucheza kamari

Mchezaji wa klabu ya Manchester City, Martin Demichelis ambaye ni Mlinzi wa kati ameshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza kwa madai ya kucheza kamari.

32AB255800000578-3515286-image-a-12_1459331585397

Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 anatuhumiwa kwa kukiuka sheria 12 zinazohusiana na mechi kati ya tarehe 22 na 28 Januari 2016.

Demichelis ana hadi Aprili 5 kujibu shtaka hilo dhidi yake.

Hatahivyo hakuna pendekezo la iwapo shtaka hilo linahusiana na mechi 25 za ligi na kombe la ligi ambazo ameshiriki msimu huu.

Sheria mpya zilizoanza kutekelezwa msimu wa 2014-2015 zinamaanisha kuwa wachezaji na makocha wanazuiliwa kushiriki kucheza dau katika mechi yoyote duniani.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lina uwezo ya kumpiga faini ama hata kumpiga marufuku mtu yeyote atakayekiuka sheria.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents