Habari

Video: Dkt Mwakyembe atema cheche kwa wasanii wanaoimba siasa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amewaomba wasanii kuboresha vipaji vyao na kutojihusisha na siasa.

Waziri Mwakyembe aliyasema hayo Bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya Bajeti ya wizara yake.

“Waheshimiwa wabunge wengi wamesema Serikali inawapuuza wadau wa masuala ya ubunifu hasa baada ya kuwatumia kwenye chaguzi mbalimbali. Muheshimiwa Mwenyekiti Serikali haijawahi kuwapuuza wasanii nchini na kama nilivyosema kwenye hotuba yangu kwa kweli tumechukua hatua mbalimbali ya kuwajengea weledi na kuwatambulisha na kuwakutanisha na wadau wa maendeleo. Nitoe wito kwa baadhi ya vyama vya siasa ambao wanawachochea hawa vijana kuimba nyimbo za siasa hii ni entertainment Industry,”alisema Dkt Mwakyembe.

“Mimi naomba vijana wangu wanisikilize mimi, nawaambia wanipe mfano wa Mwanamuziki yoyote duniani (Successful) aliyewahi kufanikiwa kwa kutukana viongozi mimi nimewaambia hivyo mimi nimeenda Nigeria Psquare wasikilize wakina Tiwa Savage wasikilize wakina Davido wakina Don Jazzy, ni vijana ambao wengine wamenunua mpaka ndege very successful, embu niambie umewasikia mtu anaimba ‘Ooooh Mr president’ wewe imba nyimbo zitakazo kuletea mafanikio wewe mwenyewe kama unataka siasa nenda kagombee siasa huko kagombee kwenye nafasi yoyote huko,” alifafanua.

“Hii ni entertainment industry na sio political industry na wengi wamenielewa angalia Afrika Mashariki wakina Chameleone, ushawahi kuona Chameleon ameiimba serikali ya Uganda? Non successful Musician anafanya hivyo namfahamu mmoja tu alijifanya mwanasiasa Fela Ramson Kuti, aliishia pabaya sana, leo tuna vijana hapa kina Diamond kina AliKiba, sikiliza nyimbo zao hakuna hata moja inayoongea mambo ya kipuuzi sijui anajifanya mwanasiasa utakuwa mwanasiasa wewe mimi nachoomba kazaneni kuboresha vipaji vyenu na mimi ninawahakikishia nitawasaidia muweze kufika katika anga ya juu kabisa.”

Tazama video hapa:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents